1Basi, mimi niliye mfungwa kwa ajili ya Bwana, nawasihi mu ishi maisha yanayostahili wito mlioitiwa. 2Muwe wanyenyekevu, wapole, wenye subira, mkivumiliana ninyi kwa ninyi katika upend o. 3Muwe wepesi wa kutaka kudumisha umoja wa Roho kwa sababu ya amani inayowafunga pamoja. 4Kuna mwili mmoja na Roho mmoja, k ama mlivyoitwa mpokee tumaini moja. 5Tena kuna Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja; 6na Mungu mmoja ambaye ni Baba wa wot e, aliye juu ya wote, anayefanya kazi katika yote na aliye ndani ya yote. 7Lakini kila mmoja wetu alipewa neema kwa kadiri ya kipimo alichogawiwa na Kristo. 8Kwa hiyo Maandiko yanasema: “Alipopaa juu, aliongoza mateka wengi, na akawapa watu zawadi.” 9Maandiko yanaposema, “Alipaa juu’ 10Yeye aliyeshuka ndiye aliyepaa juu sana, kupita mbingu zote, ili apate kujaza vitu vyote. 11Yeye ndiye aliyewapa watu vipawa, wengine kuwa mitume, wengine kuwa manabii, wengine kuwa wainjilisti, na wengine kuwa wachungaji na walimu; 12wapate kuwatayarisha watu wa Mungu kwa kazi za huduma, kwa ajili ya kujenga kanisa, ambalo ni mwili wa Kristo. 13Kazi hiyo itaende lea mpaka sote tuufikie umoja katika imani na katika kumjua Mwana wa Mungu; tupate kuwa watu waliokomaa kiroho kwa kufikia kiwango cha ukamilifu wote ulio ndani ya Kristo. 14Hapo ndipo tutaacha kuwa tena kama watoto wadogo, wanaorushwarushwa huku na huko na kupeperushwa na kila upepo wa mafundisho na hila za watu wadan ganyifu. 15Badala yake, tukiambiana ukweli kwa upendo, tutakua kwa kila hali, tufanane na Kristo ambaye ndiye kichwa. 16Kutoka kwake, mwili wote ukiwa umeunganishwa na kushikamanishwa pamoja kwa viungo vyake, hukua na kujengeka katika up endo, kila sehemu ikifanya kazi yake. Maisha Mapya Ndani Ya Kristo
17Kwa hiyo nawaambia na kusisitiza katika Bwana kwamba, msiishi tena kama watu wa mataifa wasiomjua Mungu, ambao wanaon gozwa na mawazo yao yasiyofaa. 18Watu hao akili zao zimetiwa giza wasiweze kuelewa; nao wametengwa mbali na uhai wa Mungu kwa sababu ya ujinga walionao na ugumu wa mioyo yao. 19Kwa kuwa hawajali kuhusu mema na mabaya, wamekuwa sugu na kutawaliwa na uasherati, wakiwa na tamaa ya kutenda kila aina ya uchafu. 20Lakini ninyi hamkujifunza hivyo kutoka kwa Kristo, 21kama kweli mlisikia habari zake na kufundishwa kumhusu, kufuatana na kweli itokayo kwa Yesu. 22Vueni maisha yenu ya zamani muweke kando hali yenu ya asili ambayo huharibiwa na tamaa potovu. 23Nia zenu zifanywe upya 24na mvae utu upya ulioumbwa kwa mfano wa Mungu katika haki na utakatifu. 25Kwa hiyo, kila mmoja wenu aache kusema uongo, na amwambie ndugu yake ukweli, kwa maana sisi sote ni viungo vya mwili mmoja. 26Mkikasirika, msitende dhambi; msikubali kukaa na hasira kutwa nzima 27na kumpa she tani nafasi. 28Mwizi asiibe tena, bali afanye kazi halali kwa mikono yake ili aweze kuwa na kitu cha kuwapa wenye kuhitaji msaada. 29Msiruhusu maneno machafu yatoke vinywani mwenu, bali mazungumzo yenu yawe ya msaada katika kuwajenga wengine kufuatana na mahitaji yao, ili wale wanaowasikiliza wapate kufaidika. 30Na msimhuzunishe Roho Mtakatifu wa Mungu ambaye ni mhuri wenu wa uthibitisho kwa siku ya ukombozi. 31Ondoeni kabisa chuki yote, ghadhabu, hasira, ugomvi na matusi, pamoja na kila aina ya uovu. 32Muwe wema na wenye mioyo ya upendo kati yenu, na kusameheana kama Mungu alivyowasamehe kwa ajili ya Kristo. Watoto Wa Nuru