Kutenda Mema
1Wakumbushe watu kujinyenyekeza kwa watawala na watu wenye mamlaka; wawe watii na wepesi kufanya kazi yo yote halali. 2 Wakumbushe wasimtukane mtu ye yote, wasiwe wagomvi, wawe wapole na waonyeshe unyenyekevu kwa kila mtu.
3 Maana kuna wakati ambapo sisi wenyewe tulikuwa wajinga, wakaidi; tukidanganywa na daima kutawaliwa na tamaa mbaya na anasa za kila aina. Tulikuwa tukiishi maisha ya uovu na wivu, tukichukiwa na watu na kuchukiana sisi kwa sisi. 4 Lakini wakati wema na upendo wa Mungu Mkombozi wetu ulipodhihirishwa, 5 ali tuokoa, si kwa sababu ya matendo mema ya haki tuliyotenda, bali kwa sababu ya huruma yake. Alituokoa kwa kuoshwa na kuzaliwa mara ya pili na kufanywa wapya kwa njia ya Roho Mtakatifu, 6 ambaye Mungu alitumiminia kwa wingi kwa njia ya Yesu Kristo Mwokozi wetu. 7 Na tukishahesabiwa haki kwa neema yake, tupate kufanywa warithi wa uzima wa milele tunaoutumainia . 8 Neno hili ni kweli kabisa. Ninataka uyatilie mkazo mambo haya ili wale waliomwamini Mungu waone umuhimu wa kutenda mema wakati wote, maana mambo haya ni mazuri na tena ni ya manufaa kwa watu.
9 Lakini jiepushe na ubishi wa kipuuzi: mambo kama orodha ndefu za vizazi na ubishi na ugomvi juu ya sheria; haya hayana maana wala hayamsaidii mtu ye yote. 10 Mtu anayesababisha mafarakano, muonye mara ya kwanza na mara ya pili. Baada ya hapo, usijishughulishe naye tena. 11 Una jua kwamba mtu kama huyo amepotoka na tena ni mwenye dhambi ambaye amejihukumu mwenyewe.
Maagizo Ya Mwisho
12 Nitakapomtuma Artema au Tikiko kwako, jitahidi kuja Nika poli unione, maana nimeamua kukaa huko wakati wa majira ya bar idi. 13 Wahimize Zena, yule mwanasheria, na Apolo waje upesi na uhakikishe kwamba hawapungukiwi na kitu cho chote. 14 Watu wetu hawana budi kujifunza kuona umuhimu wa kutenda mema, ili waweze kusaidia watu wenye mahitaji ya lazima na maisha yao yasikose kuwa na matunda.