Yohana Mbatizaji Akatwa Kichwa
1Wakati huo, mfalme Herode alisikia habari za Yesu; 2akawaam bia watumishi wake, “Huyu ni Yohana Mbatizaji, amefufuka kutoka kwa wafu; ndio sababu nguvu za kutenda miujiza zinafanya kazi ndani yake.”
3Herode alikuwa amemkamata Yohana akamfunga na kumweka gere zani kwa sababu ya Herodia, mke wa Filipo, kaka yake. 4Kisa che nyewe ni kwamba Yohana alikuwa amemwambia Herode kuwa, “Si halali kwako kumwoa huyo mwanamke.” 5Herode alitaka sana kumwua Yohana lakini akaogopa watu kwa maana walimtambua kuwa ni nabii. 6Lakini siku ya kusherehekea sikukuu ya kuzaliwa kwa Herode, binti ya Herodia alicheza mbele ya watu walioalikwa akamfurahisha sana Herode. 7Naye akaahidi kwa kiapo kumpa huyo binti lo lote atakaloomba. 8Kwa kushawishiwa na mama yake, huyo binti akasema, “Nipatie kichwa cha Yohana Mbatizaji kwenye sinia.” 9Mfalme akajuta; lakini kwa ajili ya kile kiapo alichoapa mbele ya wageni, aliamuru kwamba ombi lake litekelezwe. 10Akaagiza Yohana Mbatizaji akatwe kichwa mle gerezani, 11na kichwa chake kikaletwa kwenye sinia, akapewa yule binti, naye akampelekea mama yake.
12Wanafunzi wa Yohana wakaja, wakauchukua mwili wake wakau zika. Kisha wakaenda, wakamwambia Yesu.
Yesu Alisha Zaidi Ya Watu Elfu Tano
13Yesu aliposikia haya, aliondoka kwa mashua akaenda mahali pasipo na watu ili awe peke yake. Lakini watu wal ipata habari, wakamfuata kwa miguu kupitia nchi kavu, kutoka mij ini. 14Yesu alipofika kando ya bahari aliona umati mkubwa wa watu, akawahurumia na akawaponya wagonjwa wao.
15Ilipofika jioni, wanafunzi wake walimfuata wakamwambia, “Mahali hapa ni nyikani, na siku imekwisha. Waage watu waondoke ili wakajinunulie chakula vijijini.” 16Yesu akasema, “Hakuna sababu ya wao kuondoka. Ninyi wapeni chakula.” 17Wakamjibu, “Hapa tuna mikate mitano na samaki wawili tu.” 18Akawaambia, “Leteni hapa.” 19Akaagiza wale watu wakae chini kwenye nyasi. Akaichukua ile mikate mitano na wale samaki wawili, akainua macho yake akatazama mbinguni, akaibariki. Akaimega ile mikate akawapa wanafunzi wake, nao wakawapa watu. 20Wote wakala, wakatosheka. Na wanafunzi wake wakakusanya vipande vipande vilivyosalia, waka jaza vikapu kumi na viwili. 21Idadi ya watu waliokula, bila kuhesabu wanawake na watoto, ilikuwa kama wanaume elfu tano.
Yesu Atembea Juu Ya Maji
22Baadaye Yesu akawaambia wanafunzi wake watangulie kwe nye mashua waende ng’ambo ya pili ya ziwa, wakati yeye anawaaga wale watu. 23Baada ya kuwaaga, akaenda mlimani peke yake kuomba. Jioni ilipofika, Yesu alikuwa hapo peke yake. 24Wakati huo ile mashua ilikwisha fika mbali, ikisukwa sukwa na mawimbi kwa sababu upepo ulikuwa mkali.
25Ilipokaribia alfajiri, Yesu akawaendea wanafunzi wake akiwa anatembea juu ya maji. 26Lakini wanafunzi wake walipom wona akitembea juu ya maji, waliingiwa na hofu kuu. Wakasema, “Ni mzimu.” Wakapiga mayowe kwa hofu. 27Lakini mara moja Yesu akasema nao, akawaambia, “Jipeni moyo. Ni mimi; msiogope.”
28Petro akamjibu, “Bwana, kama ni wewe, niambie nije kwako nikitembea juu ya maji.” 29Yesu akamwambia, “Njoo.” Basi Petro akatoka katika mashua, akatembea juu ya maji akimfuata Yesu. 30Lakini alipoona upepo mkali aliingiwa na hofu, akaanza kuzama, huku akipiga kelele, “Bwana, niokoe!”
31Mara Yesu akanyoosha mkono wake, akamshika, akamwambia, “Wewe mwenye imani haba, kwa nini ulikuwa na shaka?” 32Na walipoingia katika mashua, upepo ukakoma. 33Wote waliokuwamo katika mashua wakamwabudu wakisema, “Hakika, wewe ni Mwana wa
Yesu Awaponya Wagonjwa Genesareti
34Walipokwisha kuvuka, wakafika Genesareti. 35Watu wa eneo lile walipomtambua Yesu, walipeleka habari sehemu zote za jirani na watu wakawaleta wagonjwa wote kwake 36wakamsihi awaru husu wagonjwa waguse tu pindo la vazi lake. Na wote waliomgusa, waliponywa.