25 1 5 Mmoja alimpa talanta tano za fedha, mwingine mbili na mwingine moja; kila mmoja alipewa kwa kadiri ya uwezo wake. Kisha akasa firi. 2Watano walikuwa wajinga na watano walikuwa na busara. 3Wale wajinga walichukua taa zao bila akiba ya mafuta; 4lakini wale wenye busara walichukua taa na mafuta ya akiba. 5Bwana harusi alipoka wia wale wasichana wote walisinzia, wakalala. 6Usiku wa manane zikapigwa kelele: ‘Bwana harusi anakuja! Tokeni nje kumlaki!’ 7Wasichana wote wakaamka, wakazitengeneza taa zao. 8Wale wajinga wakawaambia wale wenye busara, ‘Tupatieni mafuta kidogo, taa zetu zinazimika.’ 9Lakini wenye busara wakajibu, ‘Pengine hayatatutosha sisi na ninyi pia, afadhali nendeni kwa wauza mafuta mkajinunulie wenyewe.’ 10Na walipokuwa wamekwenda kunu nua mafuta, bwana harusi akafika. Wale wasichana waliokuwa tayari wakaingia pamoja naye kwenye karamu ya harusi na mlango uka fungwa. 11Baadaye wale wasichana wengine pia wakaja, wakaita, ‘Bwana! Bwana! Tufungulie mlango!’ 12Bwana harusi akawajibu, ‘Nawaambieni kweli, siwajui.’ 13Kwa hiyo kesheni, kwa sababu hamjui siku wala saa”
Watumishi Watatu Walioachiwa Talanta
14“Pia Ufalme wa mbinguni utafananishwa na mtu aliyekuwa anasafiri, akawaita watumishi wake na kuwakabidhi mali yake.
16“Yule aliyepewa talanta tano alikwenda mara moja kuzifa nyia biashara akapata talanta tano zaidi. 17Yule aliyepewa tal anta mbili akafanya hivyo hivyo, akapata mbili zaidi. 18Lakini yule mtumishi aliyepata talanta moja, alikwenda akachimba shimo akaifukia huko.
19“Baada ya muda mrefu yule bwana wa hao watumishi alirudi akakagua hesabu za fedha zake alizowaachia. 20Yule mtumishi aliyepokea talanta tano akaja, akaleta talanta tano zaidi. Akasema, ‘Bwana ulinikabidhi talanta tano, hizi hapa, nimezalisha talanta tano zaidi.’ 21Bwana wake akamwambia, ‘Umefanya vizuri sana, mtumishi mwema na mwaminifu; umekuwa mwaminifu katika machache; nitakupa mamlaka juu ya vitu vingi zaidi. Njoo ufurahi pamoja na bwana wako.’ 22Yule mwenye talanta mbili naye akaja. Akasema, ‘Bwana, ulinikabidhi talanta mbili. Nami nimepata faida, hizi hapa talanta mbili zaidi.’ 23Bwana wake akajibu, ‘Umefanya vizuri sana, mtumishi mwema na mwaminifu; umekuwa mwaminifu katika machache, nami nitakupa mamlaka juu ya vitu vingi zaidi. Njoo ufurahi pamoja na bwana wako.’
Njoo ufurahi pamoja na bwana wako.’
24Kisha yule mtumishi aliyepokea talanta moja akaja, akasema, ‘Bwana, nilijua kwamba wewe ni mtu mgumu, unavuna ambapo hukupanda na kukusanya ambapo hukutawanya mbegu. 25Kwa hiyo niliogopa, nikaenda nikaificha talanta yako ardhini. Hii hapa mali yako.’
26Lakini Bwana wake akamjibu, ‘Wewe mtumishi mwovu na mvivu! Ulijua kwamba ninavuna nisipopanda na kukusanya nisipota wanya mbegu? 27Mbona basi hukuweka fedha zangu benki ili nita kaporudi nizichukue na faida yake? 28Mnyang’anyeni hiyo talanta mumpatie yule mwenye talanta kumi.’ 29Kwa maana kila mtu mwenye kitu ataongezewa, naye atakuwa navyo kwa wingi. Lakini kwa yule asiye na kitu, hata kidogo alicho nacho atanyang’anywa. 30‘Mtupeni huyo mtumishi asiyefaa nje kwenye giza, huko kuta kuwa na kilio na kusaga meno.’ ”
Kondoo Na Mbuzi
31“Mwana wa Adamu atakapokuja katika utukufu wake pamoja na malaika wote, ataketi katika kiti chake cha utukufu cha enzi. 32Watu wa mataifa yote watakusanyika mbele yake, naye atawaten ganisha kama mchungaji anavyotenganisha kondoo na mbuzi. 33Atawaweka kondoo upande wa kulia na mbuzi upande wa kushoto. 34Ndipo Mfalme atawaambia wale walioko upande wa kulia, ‘Njooni ninyi mliobarikiwa na Baba yangu, urithini Ufalme mlioandaliwa tangu mwanzo wa dunia. 35Kwa maana nilikuwa na njaa mkanipa chakula; nilikuwa na kiu mkanipa kitu cha kunywa; nilikuwa mgeni mkanikaribisha; 36nilikuwa sina nguo, mkanivisha; nilikuwa mgonjwa mkaja kunitazama; na nilikuwa kifungoni mkaja kunitembe lea.’
37“Kisha wale wenye haki watamjibu, ‘Bwana, ni lini tuli kuona na njaa tukakulisha au ukiwa na kiu tukakupa kitu cha kunywa ? 38Na ni lini tulikuona ukiwa mgeni tukakukaribisha au ukihitaji nguo tukakuvisha? 39Na ni lini tulikuona ukiwa mgonjwa au ukiwa kifungoni tukakutembelea?’
40“Mfalme atajibu, ‘Ninawaambia kweli, kwa jinsi ambavyo mlivyomfanyia mmojawapo wa hawa ndugu zangu walio wadogo, mlini fanyia mimi.’
41“Kisha atawaambia wale walio kushoto kwake, ‘Ondokeni kwangu ninyi mliolaaniwa, nendeni katika moto wa milele alioan daliwa shetani na malaika zake. 42Kwa maana nilikuwa na njaa hamkunipa chakula; nilikuwa na kiu na hamkunipa kitu cha kunywa; 43nilikuwa mgeni wala hamkunikaribisha; nilikuwa uchi hamkuni vika; na nilikuwa mgonjwa na gerezani nanyi hamkuja kunitazama.’
44“Ndipo wao pia watajibu, ‘Bwana ni lini tulikuona ukiwa na njaa au kiu, au ukiwa mgeni au ukihitaji nguo, au ukiwa mgonjwa na kifungoni na hatukukuhudumia?’
45“Naye atawajibu, ‘Nawaambieni kweli, kwa jinsi ambavyo hamkumfanyia mmojawapo wa hawa ndugu zangu walio wadogo, hamkuni fanyia mimi.’
46“Basi hawa wataingia katika adhabu ya milele, lakini wale wenye haki wataingia katika uzima wa milele.”