Askari Mwaminifu Wa Kristo Yesu
1Basi, wewe mwanangu, uwe imara katika neema iliyomo ndani ya Kristo Yesu. 2 Na mambo ambayo ulinisikia nikiyasema mbele ya mashahidi wengi, uwakabidhi watu waaminifu ambao wataweza kuwa fundisha watu wengine pia. 3 Vumilia mateso pamoja nasi kama askari mwema wa Kristo Yesu. 4 Hakuna askari ambaye akiwa vitani hujishughulisha na mambo ya kiraia kwa sababu nia yake ni kumrid hisha yule aliyemwandika kuwa askari. 5 Hali kadhalika mwanar iadha hawezi kupewa tuzo kama hakufuata masharti. 6 Mkulima mwe nye bidii ndiye anayestahili kupata fungu la kwanza la mavuno. 7 Yatafakari haya ninayokuambia, kwa maana Mungu atakupa ufahamu katika mambo yote.
8 Mkumbuke Yesu Kristo aliyefufuliwa kutoka kwa wafu, aliyez aliwa katika ukoo wa Daudi. Hii ndio Injili yangu ninayoihubiri. 9 Nami ninateseka kwa sababu ya Injili hii nikivaa minyororo kama mhalifu. Lakini neno la Mungu halikufungwa minyororo. 10 Kwa hiyo ninavumilia taabu zote kwa ajili ya wateule wa Mungu, kusudi na wao pia wapokee wokovu uliomo ndani ya Kristo Yesu pamoja na utukufu wake wa milele.
11 Neno hili ni kweli kabisa: kwamba kama tumekufa pamoja naye, tutaishi pamoja naye pia. 12 Kama tukivumilia, tutatawala pamoja naye pia; kama tukimkana, naye pia atatukana. 13 Tusipo kuwa waaminifu, yeye huendelea kuwa mwaminifu kwa maana hawezi kujikana mwenyewe.
Mfanyakazi Mwenye Kibali Mbele Za Mungu
14 Wakumbushe mambo haya na uwaamuru mbele za Bwana waache kubishana juu ya maneno. Hii haiwasaidii cho chote bali huwaanga miza wanaowasikiliza. 15 Jitahidi kujidhihirisha mbele za Mungu kama mtu aliyepata kibali chake, mfanyakazi asiyekuwa na sababu yo yote ya kuona aibu, ambaye hulitumia neno la kweli kwa usa hihi. 16 Jiepushe na maneno ya kipuuzi, yasiyo ya kimungu, kwa maana hayo huwavuta watu mbali na Mungu zaidi na zaidi. 17 Mafundisho yao yataendelea kuenea kama donda ndugu. Kati yao wamo Himenayo na Fileto 18 ambao wametanga tanga na kuiacha kweli wakisema kwamba ufufuo umekwishapita. Wanapotosha imani ya baadhi ya watu. 19 Lakini msingi thabiti wa Mungu umesimama imara ukiwa na muhuri wenye maneno haya: “Bwana anawajua walio wake,” na tena, “Kila anayelitaja jina la Bwana aache uovu.”
20 Katika nyumba ya kifahari kuna vyombo vya dhahabu na fedha na pia vimo vyombo vya mbao na vya udongo. Baadhi ya vyombo ni vya heshima lakini vingine sio. 21 Kama mtu akijitakasa na kujitenga na visivyo vya heshima atakuwa chombo cha kutumika kwa shughuli za kifahari; chombo kilichotakaswa kimfaacho Bwana wa nyumba, ambacho ni tayari kwa matumizi yote yaliyo mema. 22 Basi, kimbia tamaa za ujana, na utafute kupata haki, imani, upendo na amani pamoja na wote wamwitao Bwana kwa moyo safi.
23 Usijishughulishe na mabishano yasiyo na maana na ya kipumbavu kwa kuwa unajua ya kwamba hayo huleta ugomvi. 24 Na tena mtumishi wa Bwana hapaswi kuwa mgomvi. Anapaswa kuwa mpole kwa kila mtu na mwalimu mwenye uwezo, na mvumilivu. 25 Anapaswa kuwaonya wale wanaompinga kwa upole, kwa matumaini kwamba Mungu anaweza kuwajalia watubu na kuifahamu kweli; 26 fahamu zao ziwarudie tena, watoke katika mtego wa shetani ambaye amewafunga wafanye kama apendavyo.