1 Petro 3

Mafundisho Kwa Wake Na Waume

1Kadhalika ninyi wake, jinyenyekezeni chini ya waume zenu, ili kama wako wasioliamini neno, wapate kuamini kwa kuvutiwa na mwenendo wa wake zao. Hawatahitaji kuambiwa neno kwa sababu wataona maisha yenu safi na ya kumcha Mungu.

Kujipamba kwenu kusiwe kwa nje, yaani: kwa kusuka nywele, kujipamba kwa dhahabu na kuvaa mavazi maridadi. Bali kujipamba kwenu kuwe katika utu wa ndani wa moyoni, kwa uzuri usioharibika, wa roho ya upole na utulivu. Uzuri wa namna hii ni wa thamani sana mbele za Mungu. Maana ndivyo walivyojipamba wanawake wata katifu wa zamani, waliomtumaini Mungu na kuwa wanyenyekevu kwa waume zao. Kama Sara alivyomtii mumewe Ibrahimu, akamwita ‘bwana’. Ninyi sasa ni binti zake Sara kama mkitenda mema pasipo kuogopa tishio lo lote.

Kadhalika ninyi waume, ishini na wake zenu kwa kuwahurumia, mkitambua ya kuwa wao ni dhaifu na hivyo muwape heshima, kwa maana ninyi ni warithi pamoja nao wa neema ya uzima. Fanyeni hivyo ili sala zenu zisizuiliwe.

Msilipe Ovu Kwa Ovu

Hatimaye, ninyi nyote muwe na nia moja, mhurumiane, mpen dane kama ndugu, muwe na mioyo ya upole na ya unyenyekevu. Msi lipe ovu kwa ovu, au tusi kwa tusi; ila barikini kwa maana hili ndilo mliloitiwa na Mungu, mpate kurithi baraka. 10 Kwa maana, “Mtu anayependa kufurahia maisha, na anayetamani kuona siku njema, basi auzuie ulimi wake usinene mabaya na midomo yake isi seme uongo. 11 Mtu huyo aepuke maovu, na atende mema; atafute amani na kuifuatilia sana. 12 Kwa maana macho ya Bwana huwaele kea wenye haki, na masikio yake husikiliza sala zao. Bali Bwana huwapa kisogo watenda maovu.”

Kuvumilia Mateso

13 Basi, ni nani atakayewadhuru ikiwa mna juhudi katika kutenda mema? 14 Lakini hata kama mtateseka kwa ajili ya haki, mtabarikiwa. Msiogope vitisho vyao wala msiwe na wasiwasi, 15 bali mioyoni mwenu mtukuzeni Kristo Bwana. Kila wakati muwe tayari kumjibu mtu ye yote atakayewauliza kuhusu tumaini lililomo ndani yenu. Lakini fanyeni hivyo kwa upole na kwa unyenyekevu.

16 Dhamiri zenu ziwe safi ili mnapotukanwa, hao wanaotukana mwenendo wenu mwema katika Kristo, waone haya. 17 Maana ni afad hali kupata mateso kwa kutenda mema kama hayo ndio mapenzi ya Mungu, kuliko kuteseka kwa kutenda maovu. 18 Maana Kristo pia alikufa mara moja tu kwa wakati wote; mwenye haki kwa ajili ya wasio na haki, ili atulete kwa Mungu. Mwili wake uliuawa lakini akafanywa hai katika roho yake. 19 Naye akiwa katika roho alik wenda kuhubiria roho zilizofungwa kifungoni. 20 Roho hizo zamani hazikutii, siku zile Mungu aliposubiri, wakati Noe alipojenga safina, watu wachache, yaani watu wanane, wakaokolewa katika ile gharika ya maji. 21 Maji hayo ni kielelezo cha ubatizo ambao sasa unawaokoa ninyi, si kwa kuondoa uchafu kwenye miili yenu, bali kama dhamana ya kuwa na dhamiri njema kwa Mungu kwa ajili ya kufufuka kwa Yesu Kristo. 22 Yeye amekwenda mbinguni, na amekaa upande wa kulia wa Mungu pamoja na malaika, mamlaka na nguvu zote zikiwa chini yake.