Yuda

Mimi Yuda, mtumishi wa Yesu Kristo, na ndugu yake Yakobo. Nawaandikia wale walioitwa na kupendwa na Mungu Baba na kulindwa na Yesu Kristo. Ninawatakieni rehema, amani na upendo tele.

Hukumu Ya Watu Wasiomcha Mungu

Wapendwa, ingawa nilikuwa na hamu kubwa kuwaandikieni kuhusu wokovu wetu, nimeona ni muhimu niwaandikieni nikiwasihi mwendelee kuipigania kwa nguvu imani ambayo Mungu amewakabidhi watakatifu mara moja tu kwa wakati wote. Hii ni kwa sababu watu wasiomcha Mungu ambao tangu zamani wamekwisha kuandikiwa hukumu hii, wamejiingiza miongoni mwenu kwa siri. Hawa ni watu ambao wanapotosha neema ya Mungu wetu na kuitumia kama kisingizio cha kutenda maovu. Wao wanamkana Yesu Kristo ambaye pekee ndiye Mkuu na Bwana wetu.

Sasa nataka kuwakumbusha jambo ambalo tayari mnalijua: kwamba, Bwana aliwaokoa watu wake kutoka Misri, lakini baadaye akawaangamiza wale ambao hawakuamini. Na malaika ambao hawaku tunza madaraka yao wakaacha maskani yao halisi; hao amewafungia gizani kwa minyororo ya milele hadi wahukumiwe katika siku ile kuu. Vivyo hivyo watu wa Sodoma na Gomora na miji ya kando kando yake ambao hali kadhalika walifanya uasherati na kujifurah isha katika matendo yaliyo kinyume cha maumbile, waliadhibiwa kwa moto wa milele kama fundisho kwa watu wote.

Ndivyo walivyo hawa watu. Ndoto zao huwaongoza wachafue miili yao, wasitii mamlaka; na watukane viumbe watakatifu walioko mbinguni. Lakini hata Mikaeli, malaika mkuu, aliposhindana na shetani kuhusu mwili wa Musa, hakuthubutu kutamka hukumu juu ya shetani, bali alisema, “Bwana akukemee!” 10 Lakini hawa watu hushutumu cho chote wasichokielewa; na yale mambo wanayotambua kwa asili, kama wanyama ambao hawawezi kujizuia kwa kutumia fikira, hayo ndio yanayowaangamiza. 11 Ole wao! Kwa maana watu hao wamefuata mfano wa Kaini, na kama Balaamu wako tayari kufanya lo lote kwa ajili ya fedha; na kama Kora wamejiangamiza wenyewe kwa kumwasi Mungu.

12 Watu hawa ni madoa katika karamu zenu za ushirika. Wanak ula nanyi bila kuwa na kiasi, wakicheka na kujishibisha na kunywa bila kujali wengine. Wao ni kama mawingu yanayochukuliwa na upepo huku na huku pasipo kuleta mvua; ni kama miti ya kiangazi iliy opukutika bila kuwa na matunda, ambayo imekufa kabisa na kung’olewa pamoja na mizizi yake. 13 Matendo yao ya aibu ni dha hiri kama vile mapovu ya mawimbi ya bahari. Wao ni kama nyota zinazotangatanga, na mahali pao ni katika lile giza kuu ambalo Mungu amewawekea milele. 14 Henoki, ambaye alikuwa wa kizazi cha saba baada ya Adamu, alitoa unabii kuhusu watu hawa akasema, “Sikilizeni! Nilimwona Bwana akija na watakatifu wake maelfu kwa maelfu 15 kutoa hukumu kwa wote na kuwaadhibu wasiomcha Mungu, kwa ajili ya matendo yao maovu waliyoyatenda na kwa ajili ya maneno makali ambayo hao waovu wasiomcha Mungu walisema juu yake.”

16 Watu hawa ni wanung’unikaji, wakaidi, wenye kufuata tamaa zao, wenye majivuno, wenye kujigamba na ambao huwasifu watu wen gine ili mambo yao yafanikiwe.

Maonyo Na Maagizo

17 Lakini ninyi wapendwa, kumbukeni yale mliyoambiwa na mitume wa Bwana wetu Yesu Kristo kwamba yatatokea. 18 Waliwaam bieni kwamba, “Katika siku za mwisho, watatokea watu watakaowad hihaki , watu wafuatao tamaa zao mbaya.” 19 Watu hawa ndio wanaosababisha mafarakano, watu wafuatao tamaa za dunia, wasio na Roho wa Mungu. 20 Lakini ninyi wapendwa, jengeni maisha yenu juu ya imani yenu takatifu; ombeni katika nguvu na uweza wa Roho Mtakatifu. 21 Jitunzeni katika upendo wa Mungu; ngojeeni rehema ya Bwana wetu Yesu Kristo itakayowafikisha kwenye uzima wa milele. 22 Wavuteni wale wenye mashaka. 23 Okoeni wengine kwa kuwany akua kutoka katika moto; wengine wahurumieni, lakini mwogope, mkichukia hata mavazi yao yaliyochafuliwa kwa tamaa zao za dhambi.

24 Basi, utukufu ni wake yeye awezaye kuwalinda msianguke na kuwafikisheni bila hatia mbele ya utukufu wake mkiwa na furaha.