2 Timotheo 4

Maagizo Ya Mwisho

1Ninakuamuru mbele za Mungu na mbele za Kristo Yesu ambaye atawahukumu walio hai na wafu; na kwa kuja kwake na ufalme wake: 2hubiri Neno; lisisitize wakati ufaao na wakati usiofaa; sadik isha, kemea, na kuonya kwa uvumilivu mkuu na mafundisho thabiti. 3Maana wakati unakuja ambapo watu hawatavumilia kusikia mafund isho yenye uzima; bali kwa kuzifuata nia zao wenyewe watajilundi kia walimu tele watakaowaambia yale ambayo masikio yao yanatamani sana kuyasikia. 4Watakataa kabisa kusikia kweli na watageukia hadithi za uongo. 5Bali wewe uwe imara, katika mambo yote, vumilia mateso, fanya kazi ya mhubiri wa Injili, timiza wajibu wote wa huduma yako.

6Maana mimi sasa ni tayari kutolewa kama sadaka, saa ya kuondoka kwangu imefika. 7Nimepigana ile vita njema, nimemaliza shindano, nimeitunza imani. 8Na sasa nimewekewa taji ya haki ambayo Bwana, mwamuzi wa haki, atanituza Siku ile; wala si mimi tu, bali na wote ambao wamengojea kwa hamu kuja kwake.

Maombi Ya Binafsi

9Jitahidi kuja kuniona upesi 10kwa sababu Dema, kwa kuu penda ulimwengu huu wa sasa, ameniacha akaenda Thesalonike. Kreske amekwenda Galatia na Tito amekwenda Dalmatia.

11Ni Luka peke yake ambaye yupo hapa pamoja nami. Mchukue Marko uje pamoja naye kwa sababu ananisaidia katika huduma yangu. 12Nimemtuma Tikiko Efeso. 13Utakapokuja, niletee lile joho nililoliacha kwa Karpo huko Troa na vile vitabu, hasa vile vya ngozi.

14Aleksanda mfua chuma alinitendea ubaya mkubwa. Mungu atamlipa kwa yale aliyonitendea. 15Wewe pia ujihadhari naye kwa sababu alipinga vikali ujumbe wetu.

16Nilipojitetea mara ya kwanza hakuna hata mmoja aliyekuwa upande wangu, kila mmoja alinikimbia. Naomba wasihesabiwe hatia kwa jambo hilo. 17Lakini Bwana alisimama nami akanitia nguvu kutangaza Habari Njema kwa ukamilifu ili watu wote wa mataifa wapate kusikia. Na niliokolewa kutoka katika kinywa cha simba. 18Bwana ataniokoa katika kila uovu na kunihifadhi mpaka niu fikie ufalme wake wa mbinguni. Atukuzwe Yeye milele na milele.

Salamu Za Mwisho

19Nisalimie Prisila na Akila na wote waliomo nyumbani kwa Onesiforo. 20Erasto alibaki Korintho. Trofimo nilimwacha akiwa mgonjwa huko Mileto.

21Jitahidi kufika huku kabla ya majira ya baridi kali. Sal amu zako kutoka kwa Eubulo, Pude, Lino, Klaudia na ndugu wote.