1Nanyi aliwafanya muwe hai, mlipokuwa mmekufa kiroho kwa ajili ya makosa na dhambi zenu. 2Hapo zamani mliishi maisha ya jinsi hiyo, mkimtii mfalme wa nguvu za anga, ambaye ndiye ile roho inayowatawala wote wanaomwasi Mungu. 3Sisi sote pia tuliishi miongoni mwao hapo zamani, tukiridhisha na kutawaliwa na tamaa mbaya za mwili na mawazo. Kwa hiyo sisi pia tulikuwa kwa asili tunastahili ghadhabu ya Mungu kama binadamu wengine wote. 4Lakini Mungu, ambaye ana huruma nyingi, kutokana na upendo wake mkuu ambao alitupenda nao, 5japokuwa tulikuwa bado tumekufa kiroho kwa sababu ya makosa yetu, alitufanya tuwe hai pamoja na Kristo Yesu. Mmeokolewa kwa neema. 6Mungu alitufufua pamoja na Kristo, akatufanya tukae pamoja naye katika makao ya mbinguni tukiwa ndani yake Kristo; 7ili katika vizazi vijavyo aonyeshe wingi wa neema yake isiyo na mfano, ambayo imedhihirishwa kwa wema wake kwetu sisi tunaoishi ndani ya Kristo Yesu. 8Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; na si kwa sababu ya matendo yenu mema. Hii ni zawadi kutoka kwa Mungu mwenyewe. 9Na kwa sababu hamkuifanyia kazi, mtu ye yote asije akajisifu juu ya wokovu wake. 10Kwa maana sisi ni matokeo ya kazi ya Mungu tulioumbwa katika Kristo Yesu, ili tuwe na matendo mema ambayo Mungu alikwisha andaa, tuishi katika hayo. 11Kwa hiyo kumbukeni kwamba ninyi ambao kwa asili ni watu wa mataifa mengine, mnaoitwa ‘wasiotahiriwa’ na wale ‘waliotahi riwa’ kwa kanuni za binadamu; 12kumbukeni kwamba wakati ule ninyi mlikuwa mmetengwa na Kristo, mkiwa mmefarakana na jumuia ya Israeli na mkiwa wageni kuhusu yale maagano ya ahadi. Mlikuwa hamna matumaini wala Mungu duniani. 13Lakini kwa kuwa mmeungana na Kristo Yesu, ninyi mliokuwa mbali zamani, sasa mmeletwa karibu kwa njia ya damu ya Kristo. 14Kwa maana yeye ndiye amani yetu; yeye aliyetufanya tuwe jamii moja, akavunjavunja ule ukuta wa uadui uliotutenga 15kwa kuifuta ile sheria na amri zake na kan uni zake alipoutoa mwili wake. Alifanya hivyo ili aumbe taifa jipya kutokana na jamii mbili: Wayahudi na watu wa mataifa, na hivyo alete amani. 16Kwa kutoa mwili wake pale msalabani, ali patanisha jamii zote mbili na Mungu; na kwa njia hiyo akaua ule uadui uliokuwepo kati yao. 17Alikuja akahubiri amani kwenu ninyi watu wa mataifa ambao mlikuwa mbali na Mungu, na pia kwa wale waliokuwa karibu na Mungu. 18Kwa maana, kwa kupitia kwake, sisi sote, Wayahudi na watu wa mataifa, tunaweza kumkaribia Baba katika Roho mmoja. 19Kwa hiyo, ninyi sasa siyo wageni tena wala wapita njia, bali mmekuwa raia halisi pamoja na watu wa Mungu na familia ya Mungu. 20Ninyi mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, na Kristo Yesu mwenyewe ndiye jiwe kuu la pembeni. 21Ndani yake yeye, jengo lote limeunganishwa pamoja na kusimam ishwa kuwa Hekalu takatifu la Mungu. 22Katika yeye ninyi pia mnajengwa pamoja ili mpate kuwa makao ambamo Mungu anaishi kwa njia ya Roho wake. Paulo, Mhudumu Kwa Watu Wa Mataifa
- Abrit | HHH
- Arabic | NAV
- Cebuano | APSD-CEB
- Chinese | CCB
- Chinese | CCBT
- Chinese | CUVS
- Croatian | CRO
- Czech | SNC
- Danish | BPH
- Dutch | HTB
- English | AMP
- English | KJV
- English | MSG
- English | NASB
- English | NIRV
- English | NIV
- English | NIVUK
- English | NLT
- Español | CST
- Español | NVI
- French | BDS
- German | HOF
- Ilonggo | HLGN
- Italian | BDG
- Japanese | JLB
- Kiswahili | SNT
- Korean | KLB
- Norwegian | LB
- Polish | SZ-PL
- Portuguese | NVI-PT
- Portuguese | OL
- Quichua | MTDS
- Romanian | NTLR
- Russian | CARS
- Russian | CARSA
- Russian | CARST
- Slovakian | NPK
- Slovakian | NRT
- Spanish | NBD
- Swedish | SVL
- Thai | TNCV
- Twi | NA-TWI