Waebrania 2

Kuzingatia Mafundisho

1Kwa hiyo, hatuna budi kuzingatia kwa makini mambo tuliyof undishwa tusije tukatanga-tanga mbali na yale tuliyosikia. 2Kwa maana kama ujumbe ulioletwa na malaika ulithibitika kuwa kweli, na kila aliyeasi na kutokutii akaadhibiwa ilivyostahili, 3sisi je? Tutaepukaje kama tusipojali wokovu mkuu namna hii? Wokovu huu kwanza ulitangazwa na Bwana, na ulithibitishwa kwetu na wale wal iomsikia. 4Mungu pia aliushuhudia kwa ishara na miujiza na maaj abu mbalimbali, pamoja na karama za Roho Mtakatifu alizogawa kufuatana na mapenzi yake.

Wokovu Umeletwa Na Kristo

5Maana Mungu hakuuweka ulimwengu ujao, tunaouzungumzia, chini ya mamlaka ya malaika. 6Bali kama inavyothibitishwa katika sehemu fulani ya Maandiko, “Mwanadamu ni kitu gani hata umfi kirie, au mwana wa binadamu ni nani hata umjali? 7Umemfanya kuwa chini kidogo ya malaika; wewe umemvika taji ya utukufu na heshima, 8umemfanya kuwa mtawala wa vitu vyote.” Mungu ali poweka vitu vyote chini ya mamlaka ya mwanadamu, hakubakiza cho chote ambacho mwanadamu hakitawali. Lakini kwa wakati huu hatuoni kama kila kitu kiko chini ya mamlaka yake. 9Lakini tunamwona Yesu, ambaye kwa muda mfupi alifanywa kuwa chini kidogo ya mal aika, sasa akiwa amevikwa taji ya utukufu na heshima kwa sababu aliteseka na kufa, ili kwa neema ya Mungu, aonje mauti kwa ajili ya watu wote.

10Kwa maana ilikuwa ni sawa kabisa kwamba Mungu, ambaye kwa ajili yake na kwa uweza wake vitu vyote vimekuwepo, amfanye Mwan zilishi wa wokovu wao kuwa mkamilifu kwa njia ya mateso, ili awalete wana wengi washiriki utukufu wake. 11Maana yule anayetakasa na wale wanaotakaswa, wote wanatoka katika uzao mmoja. 12Ndio maana Yesu haoni aibu kuwaita wao ndugu zake, akisema: “Nitalitangaza jina lako kwa ndugu zangu, katikati yao nitakusifu.” 13Na tena anasema, “Nitamwekea Mungu tumaini langu.” Na tena, “Niko hapa, mimi pamoja na watoto niliopewa na Mungu.”

Mungu.”

14Basi, kwa kuwa watoto hao wana mwili na damu, yeye pia alishiriki katika ubinadamu wao, ili kwa kufa kwake apate kumwan gamiza yule mwenye mamlaka juu ya kifo, yaani shetani; 15na hivyo awaweke huru wale ambao walikuwa utumwani maisha yao yote kwa sababu ya kuogopa kifo. 16Maana ni wazi kwamba hakuja kuwa saidia malaika bali kuwasaidia uzao wa Ibrahimu. 17Kwa sababu hii ilibidi awe kama ndugu zake kwa kila hali, apate kuwa kuhani mkuu mwenye huruma na mwaminifu katika huduma ya Mungu, ili aweze kujitoa kama sadaka kwa ajili ya dhambi za watu. 18Na kwa kuwa yeye mwenyewe ameteswa na kujaribiwa, anaweza kuwasaidia wanaoj aribiwa.