Mwenendo Wa Mkristo
1Endeleeni kupendana kama ndugu. 2Msiache kuwakaribisha wageni, maana kwa kufanya hivyo watu wengine waliwakaribisha mal aika pasipo kujua. 3Wakumbukeni waliofungwa gerezani kama vile mmefungwa pamoja nao; pia wakumbukeni wanaoteswa, kwa kuwa na ninyi bado mnaishi katika mwili.
4Ndoa iheshimiwe na watu wote, na wenye ndoa wawe waaminifu kwa wenzi wao ; maana Mungu atawahukumu wazinzi na waasherati.
5Maisha yenu yasitawaliwe na tamaa ya kupenda fedha, na mridhike na mlivyo navyo; kwa kuwa yeye mwenyewe amesema, “Sita kupungukia kamwe wala sitakuacha.” 6Kwa hiyo tunaweza kusema kwa ujasiri, “Bwana ni msaada wangu, sitaogopa kitu, mwanadamu anaweza kunifanya nini?”
7Wakumbukeni viongozi wenu, wale waliowaambia neno la Mungu. Tafakarini jinsi walivyoishi na matokeo ya mwenendo wao, mkaige imani yao. 8Yesu Kristo ni yule yule, jana, leo na hata milele. 9Msipotoshwe na mafundisho ya kigeni ya namna mbalimbali. Ni vema mioyo yenu iimarishwe kwa neema, na wala si kwa kutii mash arti kuhusu vyakula, ambavyo havina faida kwa wanaovila. 10Sisi tunayo madhabahu ambayo wale wanaohudumu katika hema ya kuabudia hawana haki ya kula vitu vilivyowekwa juu yake.
11Nyama za hao wanyama ambao damu yao huletwa na kuhani mkuu katika Patakatifu pa Patakatifu kama dhabihu ya dhambi, huchomwa nje ya kambi. 12Kwa hiyo Yesu naye aliteswa nje ya mlango wa mji ili awatakase watu kwa damu yake. 13Kwa hiyo tum wendee nje ya kambi, tukashiriki aibu aliyostahimili. 14Maana hapa hatuna mji wa kudumu, bali tunautafuta ule mji ujao.
15Basi, kwa njia ya Yesu, tuendelee kumtolea Mungu dhabihu ya sifa, yaani, matunda ya midomo ya watu wanaokiri jina lake. 16Msiache kutenda mema na kushirikiana mlivyo navyo, kwa maana sadaka kama hizi ndizo zinazompendeza Mungu.
17Watiini viongozi wenu na kufanya wanavyowaagiza. Wao wanachunga roho zenu, kama watu ambao watatoa ripoti ya huduma yao. Watiini kusudi wafanye kazi yao kwa furaha, na wala si kama mzigo, maana hiyo haitakuwa na faida kwenu.
18Tuombeeni, kwa maana tuna hakika kwamba tunayo dhamiri safi na tunapenda kufanya yaliyo sawa daima. 19Ninawasihi zaidi mniombee ili nirudishwe kwenu upesi zaidi.
Sala
20Basi, Mungu wa amani aliyemleta tena kutoka kwa wafu Bwana wetu Yesu, Mchungaji Mkuu wa kondoo, kwa damu ya agano la milele, 21awape ninyi kila kitu chema, ili mpate kutimiza mapenzi yake akifanya ndani yenu lile linalopendeza machoni pake, kwa njia ya Yesu Kristo; yeye apewe utukufu milele na milele.
Maneno Ya Mwisho
22Basi, ndugu zangu, nawasihi mpokee vema maonyo haya, maana nimewaandikia kwa ufupi.
23Napenda kuwafahamisha kwamba ndugu yetu Timotheo amefun guliwa kutoka gerezani. Akifika mapema, nitakuja naye kuwaona.
24Wasalimuni viongozi wenu wote pamoja na watu wote wa Mungu. Salamu zenu kutoka kwa ndugu wa Italia.