Tuige Mfano Wa Yesu
1Basi na sisi kwa kuwa tunazungukwa na wingu kubwa namna hii la mashahidi, tuweke kando kila mzigo mzito, na dhambi inay otusonga kwa urahisi; tupige mbio kwa ustahimilivu katika mashin dano yaliyowekwa mbele yetu. 2Tumtazame Yesu aliyeanzisha na anayekamilisha imani yetu. Yeye, kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake, alivumilia kifo cha msalaba bila kujali aibu, na sasa ameketi upande wa kulia wa kiti cha enzi cha Mungu.
3Mtafakarini yeye aliyestahimili uadui wa namna hii kutoka kwa wenye dhambi; msije mkachoka wala kufa moyo. 4Katika kushin dana kwenu na dhambi, bado hamjapigana na majaribu kiasi cha kufikia hatua ya kumwaga damu yenu. 5Je, mmekwisha sahau yale maneno ya kuwatia moyo, yanayowataja kama wana? “Mwanangu, usid harau nidhamu ya Bwana, wala usife moyo anapokukanya. 6Maana Bwana huwaadhibu wale awapendao na humpiga kila anayemkubali kuwa ni mwanae.”
7Vumilieni mateso kama mafunzo. Mungu anawatendea kama wanawe. Maana ni mwana yupi asiyeadhibiwa na baba yake? 8Kama mtaachiwa bila kuwa na nidhamu, na kila mtu hufundishwa kuwa na nidhamu, basi ninyi ni wana haramu, si wanawe wa halali. 9Zaidi ya hayo, baba zetu waliotuzaa walituadhibu nasi tukawaheshimu kwa ajili hiyo. Je, si inatupasa kujinyenyekeza zaidi kwa baba wa roho zetu ili tuishi? 10Baba zetu wa hapa duniani walituadhibu kwa muda mfupi kama wao wenyewe walivyoona kwamba inafaa. Lakini Mungu anatuadhibu kwa faida yetu, ili tuushiriki utakatifu wake. 11Adhabu yo yote huonekana kuwa kitu cha kuumiza na kisichofu rahisha wakati ule inapotolewa. Lakini baadaye, matunda yake kwa wale waliofundishwa kwa nidhamu hiyo, ni haki na amani.
12Kwa hiyo imarisheni mikono yenu iliyolegea na magoti yenu yaliyo dhaifu. 13Nyosheni njia za miguu yenu ili mguu ulioumia usilemae, bali upone.
14Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na utaka tifu, ambao bila kuwa nao, hakuna mtu atakayemwona Bwana. 15Angalieni sana mtu ye yote asishindwe kupata neema ya Mungu, na muwe waangalifu pasizuke chuki ambayo, kama mmea wenye sumu, inaweza kukua ikaleta matatizo na kuwachafua wengi. 16Hakik isheni kwamba miongoni mwenu hamna mwasherati au mtu asiyemcha Mungu. Kama Esau, ambaye kwa ajili ya mlo mmoja, aliuza haki yake ya kuwa mzaliwa wa kwanza. 17Maana mnafahamu ya kwamba baadaye, alipotaka kurithi ile baraka aliyokuwa apewe, alikataliwa, maana hakupata nafasi ya kutubu, ingawa aliitafuta kwa machozi.
18Hamkuja kukaribia mlima ambao unaweza kuguswa, na ambao unawaka moto; wala hamkuja kwenye giza, huzuni na dhoruba, 19na mlio wa tarumbeta na sauti ikisema maneno kwa kiasi ambacho wale walioisikia waliomba wasiambiwe neno lingine zaidi. 20Kwa maana hawakuweza kustahimili amri iliyotolewa: “Kama hata mnyama atag usa mlima huu, atapigwa mawe.” 21Kwa hakika waliyoona yalikuwa ya kutisha kiasi kwamba Mose alisema, “Ninatetemeka kwa hofu.” 22Lakini ninyi mmekuja kwenye Mlima wa Sioni, na kwenye mji wa Mungu aliye hai, Yerusalemu ya mbinguni, ambapo wamekusanyika kwa shangwe maelfu na maelfu ya malaika. 23Mmefika kwenye kanisa la wazaliwa wa kwanza wa Mungu ambao majina yao yameandikwa mbin guni. Mmekuja mbele ya Mungu, hakimu wa watu wote, na mbele ya roho za watu wenye haki, waliofanywa wakamilifu. 24Mmefika kwa Yesu, msuluhishi wa agano jipya, na kwa damu ile iliyonyunyizwa, inenayo maneno mema kuliko damu ya Abeli.
25Angalieni, msije mkamkataa yeye anenaye. Ikiwa hawa kuepuka adhabu walipomkataa yeye aliyewaonya hapa duniani, sisi tutaepukaje tukimkataa yeye anayetuonya kutoka mbinguni? 26Wakati ule sauti yake ilitetemesha dunia, lakini sasa ameahidi, “Kwa mara moja tena nitatetemesha si nchi tu bali na mbingu pia.”
27Maneno haya, “Kwa mara moja tena,” yanaonyesha kwamba vile vinavyotetemeshwa vitaondolewa, yaani vyote vilivyoumbwa, kusudi vibaki vile tu visivyoweza kutetemeshwa.
28Kwa hiyo, tuwe na shukrani kwa kuwa tumepokea ufalme usioweza kutetemeshwa, na hivyo tumwabudu Mungu kwa namna itakay ompendeza, kwa unyenyekevu na kicho; 29maana Mungu wetu ni moto unaoteketeza.