Viongozi Katika Kanisa
1Neno hili ni kweli, kwamba mtu akitaka kuwa askofu, anata mani kazi njema. 2Basi, askofu awe mtu asiye na lawama. Awe mume wa mke mmoja, mwenye kiasi na busara, mtaratibu, mkarimu na aju aye kufundisha. 3Asiwe mlevi, wala mgomvi bali awe mpole; asiwe mbishi wala mtu apendaye fedha. 4Aweze kuisimamia nyumba yake vizuri akiwafanya watoto wake kuwa wanyenyekevu na wenye heshima katika hali zote. 5Kwa maana kama mtu hawezi kuitawala nyumba yake mwenyewe atawezaje kuliangalia kanisa la Mungu? 6Asiwe mtu aliyeongoka karibuni asije akajiona na kuhukumiwa kama shetani alivyohukumiwa. 7Kadhalika, awe mwenye sifa njema kati ya watu wa nje ya kanisa, asije akalaumiwa na kuanguka katika mtego wa shetani.
Wasaidizi Katika Kanisa
8Vivyo hivyo mashemasi wawe wenye kuheshimika, si wenye kauli mbili au wanywaji mno wa divai au wenye tamaa ya fedha. 9Wanapaswa kuizingatia ile siri ya imani kwa dhamiri safi. 10Ni lazima wapimwe kwanza na wakionekana kuwa wanafaa basi waruhusiwe kutoa huduma ya ushemasi. 11Hali kadhalika, wake zao wawe wenye kuheshimika, si wasengenyaji bali wenye kiasi na waaminifu katika mambo yote. 12Shemasi awe mume wa mke mmoja; na aweze kuwatawala watoto wake na jamaa yake vema. 13Watu wanaotoa huduma njema ya ushemasi hujipatia heshima kubwa na uha kika mkubwa katika imani yao kwa Kristo Yesu.
14Ninakuandikia mambo haya sasa ingawa natarajia kuwepo pamoja nawe karibuni, 15ili kama nikicheleweshwa, upate kujua jinsi watu wanavyopaswa kuenenda katika nyumba ya Mungu, ambayo ni kanisa la Mungu aliye hai, nguzo na msingi wa kweli. 16Bila shaka yo yote, siri ya dini yetu ni kuu: Alidhihirishwa katika mwili wa kibinadamu, alithibitishwa katika Roho, alionwa na mal aika, alihubiriwa kati ya mataifa, akaaminiwa ulimwenguni, aka chukuliwa juu katika utukufu.