Ombi Kuhusu Maombezi
1Hatimaye, ndugu wapendwa, tuombeeni ili neno la Mungu lienee upesi na kukubaliwa kama ilivyokuwa kwenu. 2Ombeni pia kwamba tuokolewe kutokana na watu waovu na wasio na haki, kwa maana si watu wote wanaamini. 3Lakini Bwana ni mwaminifu. Ata waimarisheni na kuwalinda kutokana na yule mwovu. 4Nasi tuna tumaini kubwa kwa Bwana juu yenu, kwamba mnafanya na mtaendelea kufanya yale tuliyowaagiza. 5Bwana aielekeze mioyo yenu kwenye upendo wa Mungu na katika ustahimilivu wa Kristo.
Onyo Kuhusu Uvivu
6Ndugu wapendwa, katika jina la Bwana Yesu Kristo, tuna waagiza mjitenge na kila ndugu ambaye ni mvivu na ambaye haishi kufuatana na maagizo tuliyowapeni. 7Maana ninyi wenyewe mnafa hamu jinsi mnavyopaswa kuiga mfano wetu. Sisi hatukuwa wavivu tulipokuwa nanyi 8wala hatukula chakula cha mtu ye yote pasipo kulipa. Bali tulifanya kazi kwa juhudi usiku na mchana ili tusimlemee mtu ye yote kati yenu. 9Hatukufanya hivi kwa sababu hatukuwa na haki ya kupata msaada wenu, bali tulitaka tuwape mfano wa kuiga. 10Maana tulipokuwa pamoja nanyi tuliwapa amri hii: “Ikiwa mtu hatafanya kazi, basi asile.”
11Tumesikia kwamba baadhi yenu ni wavivu, hawana shughuli maalumu isipokuwa kusengenya wenzao. 12Sasa tunawaagiza na kuwaonya watu hao katika jina la Bwana Yesu Kristo, wafanye kazi ili wajipatie chakula wanachokula. 13Ndugu wapendwa, ninyi msi choke kutenda mema.
14Ikiwa mtu atakataa kutii maagizo tunayotoa katika barua hii, mwangalieni vema mtu huyo, mjitenge naye, ili apate kuona aibu. 15Lakini msimhesabu kama adui bali mkanyeni kama ndugu.
Salamu Za Mwisho
16Sasa, Bwana wa amani mwenyewe awapeni amani nyakati zote na kwa njia zote. Bwana na awe nanyi nyote.
17Mimi, Paulo, ninaandika salamu hizi kwa mkono wangu mwe nyewe. Hii ndio alama ya utambulisho katika barua zangu zote.