Kuja Kwa Bwana Na Kudhihirishwa Kwa Mwovu
1Basi, kuhusu kuja kwa Bwana wetu Yesu Kristo na kukusanyika kwetu mbele zake, tunawasihi, ndugu wapendwa, 2msifadhaike au kuwa na wasiwasi kutokana na utabiri fulani, au taarifa au barua inayosemekana kuwa imetoka kwetu, kusema eti kwamba siku ya Bwana imekwisha kuja. 3Mtu asiwadanganye kwa namna yo yote maana siku hiyo haitakuja kabla ya uasi kutokea kwanza na yule mwasi adhi hirishwe, yule ambaye mwisho wake ni kuangamizwa kabisa. 4Yeye anapinga kila ambacho watu hukiita mungu au cho chote kinachoabu diwa; naye hujiweka hata katika Hekalu la Mungu, akijitangaza mwenyewe kuwa ndiye Mungu.
5Je, hamkumbuki kuwa nilipokuwa pamoja nanyi niliwaambieni mambo haya? 6Na mnajua kinachomzuia sasa, ili adhihirishwe wakati ufaao. 7Maana ile nguvu ya siri ya uasi imekwisha anza kufanya kazi; lakini yule anayeizuia ataendelea kufanya hivyo mpaka atakapoondolewa. 8Hapo ndipo yule mwovu ataonekana, na Bwana Yesu atamwua kwa pumzi ya kinywa chake na kumwangamiza kabisa kwa ufahari wa kuja kwake. 9Kuja kwa yule mwovu kutafuata kazi ya shetani ambayo itaonyeshwa katika aina zote za ishara bandia na maajabu ya uongo; 10na katika kila aina ya uovu unaotumiwa kuwadanganya wale wanaoangamia. Wanaangamia kwa sababu walikataa kuipenda kweli wapate kuokolewa. 11Ndio maana Mungu ameruhusu watawaliwe na nguvu ya udanganyifu ili waendelee kuu amini uongo; 12na ili wote wasioamini kweli bali hufurahia uovu, wahukumiwe.
Simameni Imara
13Lakini tunapaswa kumshukuru Mungu daima kwa ajili yenu, ndugu mpendwao na Bwana, maana Mungu aliwachagueni tangu mwanzo ili mwokolewe kwa kutakaswa na Roho na kwa kuiamini kweli. 14Mungu amewaitieni jambo hili kwa njia ya mahubiri yetu ya Habari Njema, ili muweze kushiriki katika utukufu wa Bwana Yesu Kristo. 15Kwa hiyo ndugu wapendwa, simameni imara na mshike sana yale mafundisho tuliyowapeni katika mahubiri yetu na kwa barua zetu.
16Bwana wetu Yesu Kristo mwenyewe na Mungu Baba yetu, ali yetupenda akatupatia faraja ya milele na tumaini jema kwa neema, 17na awafariji mioyoni mwenu na kuwaimarisheni katika kila jambo jema mnalosema au kutenda.