Maonyo Ya Mwisho Na Salamu
1Hii itakuwa ni safari yangu ya tatu kuja kwenu. “Shitaka lo lote lazima lithibitishwe na mashahidi wawili au watatu.” 2Niliwaonya wale waliotenda dhambi na wengine wote, na sasa nawaonya tena nikiwa siko nanyi kama nilivyowaonya wakati nili powatembelea mara ya pili, kwamba nikija tena sitawahurumia. 3Kwa kuwa mnataka kupata ushahidi kuwa Kristo anazungumza kupi tia kwangu, hiyo itakuwa ushahidi wangu. Yeye si mdhaifu anapow ashughulikia bali ni mwenye nguvu ndani yenu. 4Kwa maana alisu lubiwa katika udhaifu, lakini anaishi kwa nguvu za Mungu. Hali kadhalika sisi ni wadhaifu ndani yake, lakini kwa nguvu za Mungu tutaishi pamoja naye ili tuweze kuwahudumia.
5Jichunguzeni mwone kama mnashika imani yenu. Jipimeni. Je, hamtambui ya kuwa Kristo yuko ndani yenu, au pengine mmeshindwa kufikia kipimo hicho? 6Natumaini mtagundua ya kuwa sisi hatu kushindwa kufikia kipimo hicho. 7Lakini tunamwomba Mungu msije mkatenda jambo lo lote ambalo ni kosa; si ili sisi tuonekane kuwa tumeshinda bali ili ninyi mtende lililo haki, hata kama tutaone kana kuwa tumeshindwa. 8Kwa maana hatuwezi kufanya lo lote kupinga kweli, bali kuithibitisha kweli. 9Tunafurahi wakati wo wote sisi tunapokuwa wadhaifu na ninyi mkawa wenye nguvu. Tuna choomba ni kwamba mpate kukomaa katika imani. 10Nawaandikieni haya wakati nikiwa mbali ili nitakapokuja nisiwe na sababu ya kuwa mkali katika kutumia madaraka ambayo Bwana amenipa kuwa jenga, na sio kuwagandamiza. 11Hatimaye ndugu zangu, kwaherini. Sahihisheni mwenendo wenu, pokeeni ushauri wangu; sikilizaneni ninyi kwa ninyi; kaeni kwa amani. Na Mungu wa upendo na amani atakuwa pamoja nanyi. 12Salimianeni ninyi kwa ninyi kwa busu takatifu. 13Watakatifu wote wanawasalimu.