Mafundisho Kwa Wake Na Waume
1Kadhalika ninyi wake, jinyenyekezeni chini ya waume zenu, ili kama wako wasioliamini neno, wapate kuamini kwa kuvutiwa na mwenendo wa wake zao. Hawatahitaji kuambiwa neno 2kwa sababu wataona maisha yenu safi na ya kumcha Mungu.
3Kujipamba kwenu kusiwe kwa nje, yaani: kwa kusuka nywele, kujipamba kwa dhahabu na kuvaa mavazi maridadi. 4Bali kujipamba kwenu kuwe katika utu wa ndani wa moyoni, kwa uzuri usioharibika, wa roho ya upole na utulivu. Uzuri wa namna hii ni wa thamani sana mbele za Mungu. 5Maana ndivyo walivyojipamba wanawake wata katifu wa zamani, waliomtumaini Mungu na kuwa wanyenyekevu kwa waume zao. 6Kama Sara alivyomtii mumewe Ibrahimu, akamwita ‘bwana’. Ninyi sasa ni binti zake Sara kama mkitenda mema pasipo kuogopa tishio lo lote.
7Kadhalika ninyi waume, ishini na wake zenu kwa kuwahurumia, mkitambua ya kuwa wao ni dhaifu na hivyo muwape heshima, kwa maana ninyi ni warithi pamoja nao wa neema ya uzima. Fanyeni hivyo ili sala zenu zisizuiliwe.
Msilipe Ovu Kwa Ovu
8Hatimaye, ninyi nyote muwe na nia moja, mhurumiane, mpen dane kama ndugu, muwe na mioyo ya upole na ya unyenyekevu. 9Msi lipe ovu kwa ovu, au tusi kwa tusi; ila barikini kwa maana hili ndilo mliloitiwa na Mungu, mpate kurithi baraka. 10Kwa maana, “Mtu anayependa kufurahia maisha, na anayetamani kuona siku njema, basi auzuie ulimi wake usinene mabaya na midomo yake isi seme uongo. 11Mtu huyo aepuke maovu, na atende mema; atafute amani na kuifuatilia sana. 12Kwa maana macho ya Bwana huwaele kea wenye haki, na masikio yake husikiliza sala zao. Bali Bwana huwapa kisogo watenda maovu.”
Kuvumilia Mateso
13Basi, ni nani atakayewadhuru ikiwa mna juhudi katika kutenda mema? 14Lakini hata kama mtateseka kwa ajili ya haki, mtabarikiwa. Msiogope vitisho vyao wala msiwe na wasiwasi, 15bali mioyoni mwenu mtukuzeni Kristo Bwana. Kila wakati muwe tayari kumjibu mtu ye yote atakayewauliza kuhusu tumaini lililomo ndani yenu. Lakini fanyeni hivyo kwa upole na kwa unyenyekevu.
16Dhamiri zenu ziwe safi ili mnapotukanwa, hao wanaotukana mwenendo wenu mwema katika Kristo, waone haya. 17Maana ni afad hali kupata mateso kwa kutenda mema kama hayo ndio mapenzi ya Mungu, kuliko kuteseka kwa kutenda maovu. 18Maana Kristo pia alikufa mara moja tu kwa wakati wote; mwenye haki kwa ajili ya wasio na haki, ili atulete kwa Mungu. Mwili wake uliuawa lakini akafanywa hai katika roho yake. 19Naye akiwa katika roho alik wenda kuhubiria roho zilizofungwa kifungoni. 20Roho hizo zamani hazikutii, siku zile Mungu aliposubiri, wakati Noe alipojenga safina, watu wachache, yaani watu wanane, wakaokolewa katika ile gharika ya maji. 21Maji hayo ni kielelezo cha ubatizo ambao sasa unawaokoa ninyi, si kwa kuondoa uchafu kwenye miili yenu, bali kama dhamana ya kuwa na dhamiri njema kwa Mungu kwa ajili ya kufufuka kwa Yesu Kristo. 22Yeye amekwenda mbinguni, na amekaa upande wa kulia wa Mungu pamoja na malaika, mamlaka na nguvu zote zikiwa chini yake.