2 Wakorintho 12:14
Neno: Bibilia Takatifu (SNT)Na sasa niko tayari kuwatembelea kwa mara ya tatu, nami sitahitaji msaada wenu kwa sababu sitaki mnipe mali yenu, ninaowahitaji ni ninyi. Kwa kuwa si sawa watoto waweke akiba kwa ajili ya wazazi wao bali wazazi waweke akiba kwa ajili ya watoto wao.