1 Wakorintho 14:5
Neno: Bibilia Takatifu (SNT)Ningependa ninyi nyote mseme kwa lugha ngeni, lakini ningependa zaidi nyote muweze kutoa una bii kwa kuhubiri neno la Mungu. Kwa kuwa anayehubiri neno la Mungu ni mkuu kuliko anayesema kwa lugha, isipokuwa kama kuna mtu wa kutafsiri, ili kanisa zima liweze kusaidika.