Yuda 1:3
Neno: Bibilia Takatifu (SNT)Wapendwa, ingawa nilikuwa na hamu kubwa kuwaandikieni kuhusu wokovu wetu, nimeona ni muhimu niwaandikieni nikiwasihi mwendelee kuipigania kwa nguvu imani ambayo Mungu amewakabidhi watakatifu mara moja tu kwa wakati wote.