Yuda 1:12

Neno: Bibilia Takatifu (SNT)
Watu hawa ni madoa katika karamu zenu za ushirika. Wanak ula nanyi bila kuwa na kiasi, wakicheka na kujishibisha na kunywa bila kujali wengine. Wao ni kama mawingu yanayochukuliwa na upepo huku na huku pasipo kuleta mvua; ni kama miti ya kiangazi iliy opukutika bila kuwa na matunda, ambayo imekufa kabisa na kung’olewa pamoja na mizizi yake.