Wagalatia 2:16

Neno: Bibilia Takatifu (SNT)
tunafahamu kwamba mtu hawezi kuhesabiwa haki kwa kutii sheria bali kwa kumwamini Yesu Kristo. Kwa hiyo sisi pia tumemwamini Yesu Kristo ili tupate kuhesabiwa haki kwa kumwa mini Kristo, na wala si kwa kuitii sheria. Maana hakuna mtu ata kayehesabiwa haki kwa kutii sheria.