Wafilipi 4:18

Neno: Bibilia Takatifu (SNT)
Nimekwishapokea malipo yangu yote na ziada. Sasa ninavyo vitu tele kwa sababu Epafrodita amekwisha niletea zawadi zenu. Hakika zawadi hizi ni matoleo yenye harufu nzuri ya manukato inayokubaliwa na kumpendeza Mungu.