Ufunua Wa Yohana 20:4
Neno: Bibilia Takatifu (SNT)Kisha nikaona viti vya enzi. Na kwenye viti hivyo vya enzi waliketi wale waliopewa mamlaka ya kuhukumu. Pia nikaona roho za wale watu waliokatwa vichwa kwa ajili ya kumshuhudia Yesu na kwa ajili ya neno la Mungu. Wao hawakuwa wamemwabudu yule mnyama wala sanamu yake na hawakuwa wamepokea alama ya yule mnyama kwenye vipaji vya nyuso zao wala mikononi mwao. Walifufuka kutoka kwa wafu wakatawala pamoja na Kristo kwa muda wa miaka elfu moja.