Ufunua Wa Yohana 17:4
Neno: Bibilia Takatifu (SNT)Huyo mwanamke alikuwa amevaa mavazi ya rangi ya zambarau na nyekundu na kujipamba kwa dhahabu, vito vya thamani na lulu. Mkononi mwake alishika kikombe cha dhahabu kilichojaa mambo ya kuchukiza na uchafu wa uasherati wake.