Matayo 21:33

Neno: Bibilia Takatifu (SNT)
“Sikilizeni mfano mwingine: mtu mmoja mwenye shamba alilima shamba akapanda mizabibu. Akalizungushia ua, na ndani yake akachimba kisima cha kusindikia zabibu; na akajenga mnara. Kisha akalikodisha hilo shamba kwa wakulima fulani, akasafiri kwenda nchi nyingine.