Matayo 12:25

Neno: Bibilia Takatifu (SNT)
Yesu alifahamu mawazo yao, akawaambia, “Utawala wo wote ambao umegawanyika wenyewe kwa wenyewe utaanguka. Hali kadhalika mji wo wote au jamaa ye yote iliyogawanyika yenyewe kwa yenyewe haitadumu.