Marko 6:56

Neno: Bibilia Takatifu (SNT)
Na kila mahali Yesu alipokwenda, ikiwa ni vijijini, mijini na mashambani, watu waliwaweka wagonjwa wao masokoni wakamwomba awaruhusu hao wagonjwa angalao waguse pindo la vazi lake. Na wote waliomgusa, waliponywa.