Luka 5:17

Neno: Bibilia Takatifu (SNT)
Siku moja Yesu alipokuwa akifundisha, Mafarisayo na wal imu wa sheria kutoka katika kila mji wa wilaya za Galilaya, Yudea na Yerusalemu walikuwepo. Na Yesu alikuwa amejaa nguvu ya Mungu ya kuponya wagonjwa.

18-19 Kisha wakaja watu wamembeba mgonjwa aliyepooza kwe nye kitanda. Wakajaribu kumpitisha ndani wamfikishe alipokuwa Yesu, lakini wakashindwa kwa sababu ya msongamano wa watu. Basi wakampandisha juu ya paa, wakaondoa baadhi ya vigae, wakapata nafasi ya kumteremsha yule mgonjwa pamoja na kitanda chake kwa kamba, hadi mbele ya Yesu.