Luka 2:35

Neno: Bibilia Takatifu (SNT)
ili kudhi hirisha mawazo yao ya ndani. Na uchungu kama kisu kikali utaku choma moyoni.” 36-37 ,Tena, alikuwepo Hekaluni nabii mmoja mwanamke, mzee sana, jina lake Ana, binti wa Fanueli, wa kabila la Asheri. Nabii Ana alikuwa mjane wa miaka themanini na minne naye alikuwa ameolewa kwa miaka saba tu mumewe akafariki. Yeye aliishi humo Hekaluni daima, akimwabudu Mungu na kuomba na kufunga.