1 Petro 4:11
Neno: Bibilia Takatifu (SNT)Mtu akisema kitu, basi na awe kama anayesema maneno halisi ya Mungu. Mtu anayetoa huduma na ahudumu kwa nguvu apewayo na Mungu; ili katika mambo yote, Mungu atukuzwe kwa njia ya Yesu Kristo. Yeye ni mwenye utukufu na uweza, milele na milele. Amina.